text Materials
Divai Tamu ya Mkomamanga Wangu

Download Attachment (PDF) Download Attachment Wordx



Divai Tamu ya Mkomamanga Wangu

 

"Ningekunywesha divai iliyokolea, Divai mpya ya mkomamanga wangu."

- Wimbo Ulio Bora  8: 2

 

Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. ”

- Yohana 1:16


 

Msingi imara wa ushirika ukiwa uliwekwa zamani katika umoja wa milele ambao uliokaa katikati ya Kristo na wateule wake, ilihitaji tu wakati wa kufaa ili ijidhihirishe yenyewe katika maendeleo yenye kutenda. Bwana Yesu alijifurahisha mwenyewe milele na wanadamu na siku zote alisimama tayari kudhihirisha na kuwasilisha furaha hiyo kwa watu wake, lakini hawakuwa na uwezo wa kurudisha mapenzi Yake au kufurahia ushirika wake, wakiwa wameanguka katika hali mbaya na ya kuaibisha, ya kwamba walikuwa wafu kwake na wasiojali kuhusu yeye. Kwa hivyo ilikuwa ni lazima ya kwamba kitu kifanyike kwa ajili yao na ndani yao kabla ya kuwa na mazungumzo na Yesu au kuhisi mapatano na Yeye.

 

Matayarisho haya yakiwa kazi ya neema na matokeo ya umoja uliotangulia, Yesu aliamua ya kwamba, hata katika maandalizi ya ushirika, inapaswa kuwa na ushirika. Ikiwa ni lazima waoshwe kabla ya kubadilishwa kabisa na Yeye, angeongea nao katika kuoshwa. Na ikiwa lazima wasitawishwe na zawadi kabla ya kupatana kabisa na yeye, Angeongea nao katika kupeana. Kwa hivyo ameanzisha ushirika katika kushirikisha neema yake na katika kuishiriki.

 

Utaratibu huu wa ushirika ambao tumeuita, "Ushirika wa Mawasiliano" na tunadhani ya kwamba maoni machache yatathibitisha ya kwamba hatukimbii mbele ya thibitisho la Maandiko.

Current Raiting:
tick image
To leave a comment, log in