text Materials
Neno kutoka kwa mdomo wa Mpendwa - Yohana 13:10

Download Attachment (PDF) Download Attachment Wordx



Neno kutoka kwa mdomo wa Mpendwa

 

"Nanyi mmekuwa safi." - Yohana 13:10


 

KAMA ngozi ya Gideoni ilikuwa imejaa umande ili ya kwamba aweze kukamua unyevu, ndivyo wakati mwingine maandiko yatakavyokuwa  wakati Roho Mtakatifu atakubali kuwatembelea watumishi wake kupitia maneno yake. Maneno haya ya Mwokozi wetu kwa wanafunzi wake ya mekuwa kama mkate mdogo mwebamba uliotengenezwa pamoja na asali kwa ladha yetu na hatuna shaka inaweza kuonja utamu sawa kwa wengine.

 

Angalia kwa uangalifu sana,rafiki wapendwa, kile ambacho ni sifa ambayo hapa imepewa wanafunzi wapendwa wa Bwana, "Nanyi mmekuwa safi." Hii ni baraka ya zamani sana, kwa haraka sana ilipotezwa na wazazi wetu wa kwanza. Huu ni uwezo, upotevu ambao unamfungia mwanadamu nje ya Paradiso na kuendelea kuwafungia wanadamu wasiingie mbinguni.

Kutaka usafi katika moyo na mikono huwahukumu wenye dhambi kufukuzwa mbali na Mungu na kunajisi matoleo yao yote. Kuwa safi mbele za Mungu ni hamu ya kila mtu mwenye majuto na tamaa ya juu sana ya mwamini aliye enda mbele zaidi. Ni ile sherehe zote na kutawadhwa kwa sheria hakuwezi kamwe kutoa na kile Mafarisayo pamoja na madai yao yote hawawezi kufikia. Kuwa safi ni kuwa kama vile malaika walivyo, kama vile watakatifu waliotukuzwa walivyo, naam, kama vile Baba mwenyewe alivyo.

 

Kukubalika na Bwana, usalama, furaha, na kila baraka kila wakati huenda na usafi wa moyo na ye yote aliye nayo hawezi kukosa mbinguni. Inaonekana kuwa hali ya juu sana kuhesabiwa kwa wanadamu, lakini, kwa midomo yake Yeye ambaye hakuweza kukosa, wanafunzi walisemekana, bila neno la kuwezesha au neno liongezalo maana la cheo, kuwa "safi", hio ni kusema, walihesabiwa haki kamili mbele ya usawa wa milele na walionekana kuwa huru kutokana na uchafu wowote.


.......... ......... ......... 




Current Raiting:
tick image
To leave a comment, log in